Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi amesema suala la kijinsia ni suala la maendeleo na Dunia yote ikiwemo Tanzania inazungumza na kijadili usawa wa kijinsia na hii yote ni kwasababu hata kama uko na watoto watano na kama ndani ya hao watoto hao wawili ni wakike na watu niwa kiume watakaokwenda shule ni wale wa kiume na wale wa kike watafanya kazi za nyumbani na kusubiria kuolewa.
Liundi ameyasema hayo wakati wa akifunga warsha iliyokuwa inahusu Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia kwa Madiwani, maafisa Mipango na Bajeti, Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa madawati ya Jinsia kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wawakilishi kutoka ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Halmshauri za wilaya ya Kishapu, Mbeya, Kasulu, Morogoro, Tarime, Same, Muheza na Moshi. Kwa Dar es salaam kuna washiriki kutoka manispaa za ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke
"Kwa Taifa ukiwekeza kwa mtoto wa kike na kiume kwa asilimia 50 kwa 50 maendeleo yatakuwa haraka sana kwasababu ya usawa wa kijinsia lakini ukiwekeza kwa jinsi moja maendeleo yatakuwa yanasuasua hii yote ni kuwa unaipa mzigo jinsi moja." alisema Liundi
Pia amsema sasa ni muda wa kutengeneza wawezeshaji ili kupunguza gharama za uendeshaji wa TGNP watakaotoa mafunzo kwa jamii pamoja na viongozi mbalimbali katika ngazi ya mtaa, kata, Wilaya na Mkoa kwa kuwa wa TGNP imewapa mafunzo hivyo nao wanaweza kuwa wakufunzi wazuri wa masuala ya kijinsia.
"Kwenye vikao vya ALAT tumekuwa tukipeleka wataalamu wetu ili kutoa mafunzi lakini kwasababu mmekuja na pendekezo la kujikita kwenye ARAT ngazi ya Mkoa basi tunaichukua na tutaiweka kwenye Bajeti zetu.Kutoka na mafunzo hayo basi kwenye vikao vya utengenezaji wa Bajeti wataweza kuongeza Bajeti yenye mrengi wa Kijinsia ambapo halmashauri ya Kishapu bado wameshika nafasi ya kwanza kwa kutumia ripoti ya TGNP hivyo halmashauri nyingine ziige mfano huo." Alisema Liundi
Naye Diwani wa Kata ya Ngerengere iliyopo Wilaya ya Morogoro Vijijini Kibena Kingu ameushukuru Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kuweza kutoa semina kwa wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutoa maoni mbadala kwenye vikao vya upangaji wa Bajeti kwenye ngazi za Halmashauri.
Pia amasema wajumbe wa warsha hiyo watakuwa mabalozi kwenyw usawa wa kijinsia hasa kwenye utengenezaji wa Bajeti yenye mrengo wa usawa wa kijinsia na pia watakwenda kutoa elimu kwa watu wanaotoa maamuzi kwenye upangaji wa Bajeti ili kuja na mabadiliko kwenye upangaji wa Bajeti zijazo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza wakati wa kufunga wa mafunzo kuhusu Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia kwa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Same, Benedict Missari akisoma mapendekezo na mkakati waliojiwekea wakatiwa kufunga kwa warsha ya Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Madiwani kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini pamoja na wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakisikiliza hituba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi alipokuwa anafunga warsha ya Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia kwa wataalam hao yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Ngerengere iliyopo Wilaya ya Morogoro Vijijini Kibena Kingu akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kuweza kutoa mafunzo ya Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia ili kujipatia ufahamu zaidi kuhusu namna ya uapangaji wa Bajeti wenye mrengo wa Kijinsia wakati wa kufunga kwa warsha hiyo iliyofanyika kuanzia terehe 21 hadi 24 Novemba 2022.
0 comments:
Post a Comment