Kijana mwenye umri wa miaka 23 amekamatwa na Polisi baada ya kumrushia mayai Mfalme wa Uingereza, King Charles III aliyekuwa akifanya ziara huko Yorkshire Kaskazini.
Kabla ya kijana huyo kutekeleza tukio hilo, Polisi walimzuia mwanaume huyo kwenye umati wa watu uliokusanyika katika eneo la Micklegate.
Kijana huyo alisikika akipiga kelele na kueleza kuwa nchi hiyo ilijengwa kwa damu ya watumwa huku akiendelea kuzomea.
Watu wengine walisikika wakisema kuwa Mungu mwokoe Mfalme na aibu juu yake kutoka kwa mwanandamanaji huyo.
Kupitia video ilizosambaa mitandaoni ilimuonesha Mfalme Charles akipeana mikono na watu mashuhuri akiwemo Meya wa eneo la Micklegate huku mayai yakiruka kuelekea kwake.
Polisi wa Yorkshire Kaskazini walisema mwanaume huyo alikamatwa kwa tuhuma za kosa hilo na tayari amewekwa chini ya ulinzi.
Tukio hilo lilitokea siku ya pili ya ziara rasmi ya kifalme huko Yorkshire, wakati ambapo Mfalme na Malkia Consort wakisafiri kwenda Doncaster.
0 comments:
Post a Comment