Watu saba ambao ni watumishi wa serikali ya wilaya ya kiteto Mkoani Manyara Idara ya afya na elimu wamefariki kwa ajali baada ya gari waliyokuwa wamepanda kugongana na gari nyingine aina ya Prado katika eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo Kiteto Mkoani Manyara.
Ajali hiyo imetokea Novemba 8,2022 eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo Kiteto Mkoani Manyara.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi ametaja majina ya waliopoteza maisha pamoja na majeruhi.
Waliopoteza maisha ni:
1.Joseph Bizuku (36) Muuguzi
2.Edward Makundi (47) Daktari
3.Agapiti Kimaro (32) Mkuu wa shule ya Esamatwa
4.Kadidi Saidi (36) Nesi
5.Celina Nyimbo 31 Mtumishi wa maabra
6 Katherine Mathei (31) Nesi
7.Nickson Mhongwa Daktari
Waliopelekwa Hospitali ya Dodoma ni
1.Method Malick (55) Dereva Prado
2.Juma Mbaruku (45) Dereba ambulance Kiteto
Waliolazwa hospitali ya Kiteto
1 Ibrahim Selemani (71)
2.Mbaraka Shabani (44)
0 comments:
Post a Comment