Tuesday, 17 September 2019

VIJANA WA CCM WATEMBELEA KITUO CHA AFYA BUNAZI MWENYEKITI WA CCM KAGERA AKIZINDUA 'MISENYI YA KIJANI'

...
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera Mhe. Costansia Buhiye ameongoza uzinduzi wa Misenyi ya Kijani leo Jumanne Septemba 17,2019 katika ofsi za chama hicho lililopo katika kata ya Kasambya wilayani Misenyi.

Kabla ya uzinduzi wa Misenyi ya Kijani viongozi na wanachama wa CCM hususani vijana wa UVCCM Misenyi, wakiongozwa na Buhiye wametembelea kituo cha afya Bunazi kwa ajili ya kuwafariji wagonjwa na kuwapatia zawadi mbali mbali ikiwemo sabuni na vinywaji na kujionea changamoto mbalimbali zilizopo kituoni hapo ikiwemo uhaba wa watumishi, uhaba wa vitanda vya wagonjwa.

Akitoa taarifa kwa viongozi hao wa CCM waliofika kituoani hapo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Bunazi,Dkt. Sweetbert Donat alisema mbali na changamoto ya uhaba wa watumishi, majengo, pamoja na vitanda.

Dkt. Donat alisema kituo hicho hupokea wagonjwa wengi licha ya kuwa na uhaba watumishi, majengo na ukosefu wa vitanda, unaosababisha watoto wawili kulala katika kitanda kimoja jambo ambalo amelitaja kuwa siyo salama kiafya.

Alisema changamoto hizo huwafanya wahudumu hao kufanya kazi kwa shida na kuomba uongozi wa CCM kuwasaidia katika kutatua changamoto zao.

Akizungumzia changamoto hizo,Buhiye  alisema kilio hicho amekipokea na atahakikisha anashughulikia na suala hilo mara moja na kuwataka wahudumu wa kituo hicho kuwapokea wagonjwa wanaofika kituoni hapo kufuata huduma za matibabu

Buhiye alitumia fursa hiyo kumpongeza mbunge wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Halima Abdallah Burembo aliyejitoa hivi karibuni kuchangia vitanda katika kituo hicho na kuwataka viongozi wengine kuiga mifano hiyo huku akiwataka viongozi wa chama hicho wilayani humo kuendelea kuwasikiliza wananchi ili kutatua kero zao.
Viongozi wa UVCCM Misenyi wakiwasili katika kituo cha afya Bunazi kwa ajili ya kuwafariji wagonjwa na kuwapatia zawadi mbali mbali ikiwemo sabuni na vinywaji na kujionea changamoto mbalimbali zilizopo kituoni hapo leo. Picha zote na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Viongozi hao wakiingia katika wodi ya wazazi.
Mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Kagera Mhe. Costansia Buhiye akisaini kitabu cha wageni.
 Kaimu mganga mfawidhi wa kituo cha afya Bunazi Dkt. Sweetbert Donat akielezea changamoto za kituo hicho.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Misenyi ya Kijani akimjulia hali mgonjwa aliyeshambuliwa na majambazi.
Diwani wa kata ya Kasambya Yusuph Hamada Mzumbe akiongea jambo na wagonjwa
Kijana wa CCM akigawa zawadi kwa wagonjwa kituoni hapo.
Bi Rehema Mtawala katibu wa wazazi Ccm wilaya ya Misenyi akikabidhi zawadi kwa wagonjwa

Picha ya pamoja ya viongozi wa CCM wakiwa eneo la nje la kituo cha afya Bunazi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misenyi Projestus Tegamaisho akiwa amekaa wakati wa uzinduzi wa Misenyi ya Kijani leo Jumanne Septemba 17,2019 katika ofsi za chama hicho lililopo katika kata ya Kasambya wilayani Misenyi.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger