
Na Francis Godwin ,Iringa
UAMUZI wa kupata ama kutopata dhamana kwa mwandishi wa habari wa kujitegemea wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa, Sebastian Atilio kujulikana Jumatatu septemba 23 mwaka huu.
Mwanahabari huyo ambae anakabiliwa na kesi ya jinai namba 208/2019 ya kutuhumiwa kwa makosa mawili la kufanya kazi ya uandishi bila kusajiliwa na bodi pamoja kuandika habari za uongo juu wananchi wa kijiji cha Ifupila Mufindi kuhamisha alifikishwa mahakamani hapo jana Septemba 18,2019.
Mwendesha mashitaka wa Jamhuri katika kesi hiyo Victor Kitomari aliiomba mahakama hiyo kusogeza mbele siku ya kusikilizwa kwa mapingamizi ya dhamana na kutoa uamuzi wa mapingamizi hayo kwa kuwa hajajiandaa.
Huku wakili upande wa utetezi Emmanuel Chengula aliiambia mahakama hiyo kuwa hoja ya wakili huyo si sahihi kwani pingamizi la dhamana walipokea septemba 11 na wao kulijibu septemba 13 mwaka huu hivyo alikuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa kwa ajili ya kusikilizwa kwa shauri hilo .
Kwani sababu ya mwendeshaji huyo kutaka kujibu kiapo kinzani ambacho hakijasilizwa si sawa na kuwa kuna mapingamizi manne ya kisheria ambayo hayajasikilizwa bado.
Hivyo aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya upande wa mashitaka kwani yanalenga kumtesa mteja wake kuendelea kusota mahabusu wakati kesi yake ya msingi ina dhamana kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo akiahirisha kesi hiyo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Edward Uforo alisema hoja zote za pande mbili ni za msingi ila katika suala hilo busara ya pande zote na mahakama inapaswa kuhusika.
"Hivyo naomba tupange Siku nyingine ya kusikiliza hoja kwa kuzingatia hoja za pande zote mbili na tupange siku ambayo haitakuwa mbali maana mtuhumiwa yupo mahabusu na kesi yake ya msingi ina dhamana "
Hivyo mahakama hiyo itatoa uamuzi mdogo baada ya kusikiliza mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya shauri la kupinga dhamana Septemba 23 ambayo itakuwa ni siku ya kutajwa kwa kesi ya msingi .
Mwanahabari huyo amerudishwa mahabusu ya gereza la Isupilo Mufindi hadi septemba 23 shauri hilo litakapofikishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya kujua hatima ya dhamana .
0 comments:
Post a Comment