Rai hiyo imetolewa leo Jumanne Septemba 17,2019 na Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius Temba wakati warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii kuhusu wanawake na uongozi wanawake katika uongozi inayolenga kuwajengea na kuwaongezea uelewa na uwezo waandishi wa habari namna ya kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi.
"Vyombo vya habari vina wajibu wa kuhabarisha wananchi kuhusu mchakato wa uchaguzi,ushiriki wa wananchi kwenye mchakato wa uchaguzi ili wawe na maamuzi sahihi",amesema Temba.
Temba ametumia fursa hiyo kuwahamasisha waaandishi wa habari kuandika habari kwa kuzingatia mrengo wa kijinsia.
"Misingi mikuu ya uandishi wa habari inatufundisha kuwa ili tuweze kufanya kazi kiuweledi ni lazima tuzingatie usahihi wa habari tunazoandika,uhuru,uwajibikaji,ubinadamu na kutopendelea upande wowote. Wakati wa kuandika habari za uchaguzi,vyombo vya habari vitumike kujenga uelewa,ujasiri na uthubutu wa wanawake katika uchaguzi",ameongeza Temba.
Warsha hiyo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa ushirikiano na UN Women imekutanisha waandishi wa habari 43 kutoka mikoa mitano ambayo ni Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora na Mara.
Lengo kuu ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kutoa taarifa zenye mrengo wa kijinsia hasa zenye kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo kubadili mitazamo na mila hasi zinazozuia ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius Temba akitoa mada kuhusu umuhimu wa wanawake kushiriki kwenye uongozi na ngazi za maamuzi na wajibu wa vyombo vya habari. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius Temba akitoa mada kuhusu umuhimu wa wanawake kushiriki kwenye uongozi na ngazi za maamuzi na wajibu wa vyombo vya habari.
Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius Temba akielezea misingi ya uandishi wa habari.
Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius Temba akielezea changamoto zinazowafanya wanawake wasishiriki kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi ambazo ni Fikra mgando,kutojiamini,ukosefu wa rasilimali na ubaguzi wa kijinsia.

Mwenyekiti wa TAMWA,Joyce Shebe ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari,Clouds Media akitoa mada kuhusu uandishi wa habari kwa mrengo wa kijinsia.

Mwenyekiti wa TAMWA,Joyce Shebe ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari,Clouds Media akitoa mada kuhusu uandishi wa habari kwa mrengo wa kijinsia.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

0 comments:
Post a Comment