Tuesday, 10 September 2019

Serikali Yatarajia Kumwaga Tsh.bilioni 33.5 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Wodi 2 Kila Hospitali 67 Za Wilaya Nchini.

...
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali inatarajia kutoa jumla ya Shilingi bilioni 33.5 kwa ajili ya kujenga wodi 2  katika kila hospitali 67 za  wilaya zinaoendelea kujengwa nchini.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa SELEMANI JAFO  amesema hayo  wakati akikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Chamwino inayojengwa katika kijiji cha Mlowa Barabarani.
 
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo waziri JAFO amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kuwahimiza kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati.
 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameishukuru serikali kwa kuimarisha huduma za afya katika mkoa wa Dodoma.
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa CHamwino ATHUMANI MASASI amesema Ujenzi huo ulianza februari mwaka huu kwa kupokea kiasi cha shilingi bilioni 1.5 na unatarajiwa kukamilika septemba 30 mwaka huu.
 
Ujenzi wa hospitali hizo ulihusisha jengo la maabara,jengo la wagonjwa kutoka nje,jengo la kuhifadhi dawa,jengo la mama na mtoto,utawala,jengo la mionzi na la kufulia nguo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger