Serikali imemwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini kupata kwa kina hoja za Shirika hilo zinazosambaa kupitia vyombo vya habari.
Mwakilishi huyo amesisitiza kuwa WHO haijasema wala haina ushahidi wowote kuwa Tanzania kuna Ebola na itashirikiana na Serikali.
Aidha, katika mazungumzo hayo WHO imeafiki kuwa kama kuna mahitaji ya kupata taarifa zaidi kutoka Serikali ya Tanzania lazima utaratibu ulioanishwa katika miongozo ya taasisi hiyo na ambayo imeridhiwa na Serikali ifuatwe kikamilifu.
Haya yanajiri wakati shirika la madaktari wasio na mipaka Medicins Sans Frontiers MSF limelituhumu shirika la WHO kwa kutumia mfumo usiofaa wa utoaji chanjo nchini DRC likisema utaratibu wa mgao unaotumika unaruhusu virusi kujitokeza tena katika jamii ambazo tayari ugonjwa huo ulikuwa umetokomezwa na watu kulindwa kutokana na maambukizi mapya.
Shirika la WHO limekanusha madai kwamba linatoa chanjo kwa mgao na badala yake limesema linafanya kazi kwa bidii kama mashirika mengine kuutokomeza kabisa mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Shirika hilo limesema katika taarifa yake kwamba linashirkikiana na serikali ya Congo kuzifikia jamii nyingi na watu wengi kadri inavyowezekana katika maeneo yaliyoathirika na mlipuko wa ebola na wala halijaweka kiwango wala vikwazo katika utoaji wa chanjo.

0 comments:
Post a Comment