Tuesday, 17 September 2019

MUONGOZA WATALII AJIUA KWA KUJIRUSHA KWENYE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

...

Thomas Meela (58), mkazi wa Marangu anayejishughulisha kuongoza watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro amekufa baada ya kujirusha kwenye kilele cha mlima huo umbali wa mita 5,895.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 17, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amesema tukio hilo limetokea Septemba 15, 2019 katika hifadhi ya mlima huo.

Amesema huenda Meela alichanganyikiwa baada ya kupata ‘homa ya mlima’, kuamua kujirusha na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

“Meela alikuwa na safari ya siku tisa kupanda mlima Kilimanjaro na Septemba 12 mchana baada ya kufika kileleni aliwaacha wageni na kwenda kuvuta sigara lakini akiwa na mwenzake ndipo alipomwambia hawatamuona tena.”

Na Janeth Joseph, Mwananchi 

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger