Tuesday, 10 September 2019

Kuelekea mtihani Darasa la saba, DED Aagiza kuvunja makundi yote Ya Whatsaap

...
Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma imevunja makundi yote ya ‘WhatsApp’ ya waratibu elimu msingi ili kuepuka udanganyifu katika mitihani ya darasa la saba inayofanyika kesho na keshokutwa.

Katika barua hiyo iliyoandikwa kwa waratibu kata elimu wote Agosti 19, 2019 na kusainiwa na Josephat Ambilikile kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo imewataka waratibu elimu kata wote kuvunja makundi hayo.

Makundi hayo ni yale yanayotumika kutoa au kupokea taarifa zozote zinahusiana na utendaji wa taaluma.

Ambilikile amesema pia ofisi imebaini kuwepo kwa makundi ya WhatsApp katika halmashauri hiyo  yanayotoa taarifa mbalimbali za kielimu na kijamii.



Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger