Thursday, 5 September 2019

KASHASHA APATA USHINDI MNONO NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA BUKOBA

...
Mhe. Deogratias Kashasha 

Na Lyidia Lugakila - Malunde 1 blog

Diwani wa kata Kishanje, Mhe. Deogratias Kashasha amefanikiwa kutetea tena kiti cha  Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba.


Uchaguzi huo umefanyika leo Septemba 5,2019 katika kikao cha baraza la madiwani kwa ajili ya kufunga mwaka 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Awali mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba,Mhe. Hashim Murshid Ngeze aliyataja majina ya wajumbe walioomba nafasi ya kugombea nafasi hiyo kuwa ni Bwana Deogratias Kashasha ambaye ni Diwani wa kata ya Kishanje (CCM) na Rwekaza Deusdedith diwani wa kata ya Katoma (Chadema).

Kufuatia uchaguzi huo,Mhe. Deogratias Kashasha ameibuka mshindi nafasi ya makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba kwa kupata kura 28 dhidi ya mpinzani wake Rwekaza Deusdedith aliyepata kura kura 7 ambapo jumla ya wapiga kura walikuwa ni 35.

Kashasha amewashukuru madiwani hao kwa kumchagua kutetea kiti hicho na kuahidi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu ili kutekekeza ilani ya Chama Cha mapinduzi CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Kushoto ni Mhe. Deogratias Kashasha (CCM) akiwa na mgombea mwenzake nafasi ya makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Bukoba,Mhe. Rwekaza Deusdedith (CHADEMA)
Mhe. Deogratias Kashasha (CCM) akijipigia kura wakati wa uchaguzi nafasi ya makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Bukoba leo
Mhe. Rwekaza Deusdedith (CHADEMA) akijipigia kura akijipigia kura wakati wa uchaguzi nafasi ya makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Bukoba leo






Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger