Tuesday, 24 September 2019

Jinsi Wachawi Wanavyowarubuni Watu

...
Hakuna  uchawi  wowote  ule  chini  ya  jua  ambao  unaweza kufanya  kazi  kwenye  maisha  ya  mtu  bila  ridhaa  ya  mtu  huyo.


Maneno  mabaya  ambayo  umekuwa  ukitamkiwa  na  watu  wengine  na  kuyasikia  halafu  ukakaa  kimya  bila  kuyakataa  kwa  maneno  au  bila  kuyafuta ndo chanzo cha kujiumiza mwenyewe .   

Mtu  akikutamkia  maneno  mabaya  iwe  kwa  kukusudia  ama  kwa  bahati  mbaya, usiyakubali  hata  kama  anakutolea  mfano  tu.  

Yakatae  na  uyafute  papo  hapo  na  yeye  akiwa  anasikia  au  kama  utashindwa  kufanya  hivyo  basi  hakikisha  baadae  unayakataa  na  kuyafuta  maneno  hayo  kwa  maneno. 

 Ipo mifano  mingi  sana  kuna  watu  walitamkiwa  maneno  mabaya tena  ya  kawaida  kabisa  na  hawakuyafuta  na  miaka  mingi  baadae  maneno  hayo  waliyo  tamkiwa  yamewatokea.

Mifano :  Kuna  jamaa  mmoja  miaka  miwili  baada  ya  kumaliza  chuo na  kupata  kazi, alikutana  na  mtu ambae  walisoma  wote  chuo.  


Huyu  jamaa  alikuwa  amebadilika, amenenepa  na  mwili  umeongezeka. Sasa  katika  maongezi  yao  huyo  mwenzake  akamwambia “ Kaka  kwa  mwili  huu, muda  si  mrefu  madaktari  wataanza  kukukataza  kutumia  baadhi  ya  vyakula “  Yeye  hakujibu  chochote  akawa  anacheka  tu.   Mwisho  wa  siku  miaka  kadhaa  baadae , jamaa akapatwa  na  presha  na  kisukari  na  sasa  hivi  kweli  hatumii  baadhi  ya  vyakula.


Endelea kuisoma hapa << HAPA>>


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger