Sunday, 15 September 2019

Iran yazikanusha shutuma za Marekani

...
Wizara ya mambo ya nje ya Iran imezipuuza shutuma za Marekani kwamba inahusika na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika vituo vya mafuta vya Saudi Arabia. 

Wizara hiyo imesema madai hayo hayana ''maana'', ikisema hicho ni kisingizo kinachotumiwa kutaka kulipiza kisasi dhidi ya jamhuri hiyo ya Kiislamu. 

Msemaji wa wizara hiyo, Abbas Mousavi amenukuliwa akisema shutuma kama hizo hazieleweki na hazina maana na kwamba zinakusudiwa kuhalalisha hatua za kuchukuliwa hapo baadae dhidi ya Iran.

 Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo aliishutumu Iran kuhusika na mashambulizi hayo yaliyofanyika jana. Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen wamedai kuhusika na mashambulizi katika vituo hivyo vya mafuta.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger