Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran amesema shambulio lolote dhidi ya nchi yake, kufuatia hujuma dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia litasababisha vita kamili na kuongeza mvutano katika Guba ya uajemi.
Tamko hilo la waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammed Javad Zarif, limewakilisha onyo kali la Iran katika kipindi kirefu cha kiangazi, kilichogubikwa na mashambulio na matukio kadhaa ya kukanganya kufuatia kuporomoka kwa makubaliano yake ya nyuklia na mataifa yalio na nguvu duniani baada ya rais Donald Trump kuiondoa Marekani katika makubaliano hayo.
Tamko lake hilo pia linaangaliwa kama jibu kwa Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo ambaye siku moja iliyopita alipokuwa akielekea Saudi Arabia aliyataja mashambulio hayo kama "tukio la vita.”
Alipoulizwa na shirika la habari la CNN ipi athari ya shambulio la Marekani na Saudi Arabia kwa taifa lake, Zarif alisema anatoa taarifa muhimu kwamba Iran isingelipenda kuingia katika majibizano ya kijeshi lakini pia akasema hawatofumba macho kulilinda taifa la Jamhuri ya Iran.
Ameongeza kuwa vikwazo vyovyote vilivyowekwa na Marekani kwa taifa lake baada ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia, inabidi viondolewe kabla ya kufanyika majadiliano ya aina yoyote, huku akisema Marekani imefanya kila iwezalo lakini bado haijaifikisha Iran kuinyenyekea kwa kuipigia goti.

0 comments:
Post a Comment