Thursday, 12 September 2019

Breaking : TRENI YAPINDUKA NA KUUA WATU KADHAA

...
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika jimbo la Tanganyika huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya treni kupoteza muelekeo.

Waziri wa masuala ya kibinadamu, Steve Mbikayi ameithibitishia BBC kuwa watu 50 wanahofiwa kufariki katika ajali hiyo.

Mbikayi ameelezea ajali hiyo kuwa janga jingine na kufahamisha kuwa mutano unaendelea kuratibu usaidizi wa dharura.

Katika ujumbe kwenye Twitter, waziri Mbikayi alitoa pole kwa familia zilizoathirika na mkasa huo.

Hatahivyo gavana wa jimbo hilo amehoji idadi hiyo ya waziri ya watu waliofariki na kusema kwamba ni watu 10 waliofariki huku wengine takrian 30 wakiwa wamejeruhiwa.

Mbikayi baadaye ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wizara yake inatambua utofuati wa idadi ya waliofariki katika mkasa huo leo na wanajaribu kubaini idadi sahihi.

Duru kutoka shirika la kijamii ameiambia BBC kwamba treni hiyo ilikuwa ni ya mizigo iliyokuwa inasafriki kuelekea mji wa Kalemie.

Mkuu wa operesheni wa kampuni ya kitaifa ya reli nchini Congo, Hubert Tshiakama, ameilezea Reuters kwambamabehewa ya mbele abayo hayakuathirika na ajali hiyo yanaelekea mjini Kalemie.

"Kwa sasa hatuwezi kubaini chanzo cha ajali," amenukuliwa kusema.

Ajali za reli hutokea nchini humo kutokana na miundo mbinu ya kitambo na isiyosimamiza kisawasawa.

Chanzo- BBC
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger