Wednesday, 11 September 2019

Baba Levo Aongezewa Kifungo Gerezani

...
Diwani wa Mwanga Kaskazini(ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Revocatus Chipando maarufu “Baba Levo“ ameongezewa  kifungo Gerezani na sasa atatumikia kifungo cha Mwaka 1 na siku 2 badala ya Miezi 5 ya awali.

Hukumu hiyo imetolewa jana Septemba 10, 2019 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, baaada ya kushindwa rufaa yake ya kupinga hukumu ya awali.

Baba Levo alikata rufaa katika mahakama hiyo kupinga adhabu ya awali ya miezi mitano, kwa kosa la kumshambulia trafiki, F.8350 PC Msafiri Mponela.

Katika hukumu ya awali Baba Levo alitiwa hatiani kwa kifungu namba 240 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 chapisho la mwaka 2002 na hukumu yake kutolewa Alhamisi Agosti 1, 2019, katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga na Hakimu Mkazi Florence Ikolongo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger