Friday, 6 September 2019

Aburuzwa Mahakamani kwa kufanya ufugaji holela Mjini Kahama

...
NA SALVATORY NTANDU
Mfugaji na Mkazi wa mtaa wa Malunga katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga Yusuph Kumalija (33) leo amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kahama kwa tuhuma ya kusababisha uharibifu wa mazingira kwa ufugaji holela wa mifugo mjini.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Julius Siza Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Felix Mbisse amedai Yusuph alitenda kosa hilo septemba tano mwaka huu majira ya saa saba mchana kwa kuachia ng’ombe wake kuzurura ovyo mjini na kuharibu Mazingira.

Amesema Yusuph amekiuka sheria ya hifadhi ya mazingira ya Halmashauri ya mji wa kahama namba 4 (1) (a),(b) inayoelekeza namna ya ufugaji wa mifugo mbalimbali hapa mjini.

Amefafanua kuwa uzururaji wa mifugo hiyo hapa mjini unasababisha uharibifu wa mazingira na ni kinyume cha sheria na amekiuka kifungu cha 53 cha sheria za serikali za mitaa ya mwaka 2014.

Yusuph amekana shitaka hilo Mahakamani hapo na Shauri hilo la jinai namba 332 la mwaka huu limeahirishwa hadi septemba 20 ambapo litakapotajwa tena na upelelezi wake umekamika

Yusuph  amepewa dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger