Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za Kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mlezi wa Timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys” Dkt.Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia jana huko Umoja wa Falme za Kiarabu.
Rais wa TFF Ndugu Karia ametoa pole kwa Familia ya Dkt.Mengi,Makampuni ya IPP,Ndugu,Jamaa,Marafiki na Familia ya Mpira wa Miguu kwa msiba huo.
Amesema Dkt.Reginald Mengi amekua na mchango mkubwa katika Mpira wa Miguu mchango ambao bado ulikua unahitajika.
“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za Msiba wa Mlezi wetu wa Serengeti Boys Dkt.Reginald Mengi sote ni mashahidi kwa namna alivyojitolea katika Mpira wa Miguu kuanzia ngazi ya Klabu mpaka Timu za Taifa hakika mchango wake bado ulikua unahitajika,Kwa niaba ya TFF natoa pole kwa Familia yake,Makampuni ya IPP,Ndugu,Jamaa,marafiki na WanaFamilia ya Mpira wa Miguu” amesema Rais wa TFF Ndugu Karia.
Kabla mauti hayajamkuta Dkt.Mengi alikua ndio mlezi wa Timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys” ambapo mara ya mwisho alikua na Timu hiyo wakati ikishiriki kwenye Fainali za Afrika za Vijana U17(AFCON) zilizofanyika Tanzania na kumalizika Aprili 28,2019 Uwanja wa Taifa.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Dkt.Reginald Mengi mahala pema peponi,Amina
0 comments:
Post a Comment