Rais John Magufuli, amefichua njama anazofanyiwa Mbunge wa Mbarali, Haroub Mohamed (CCM), zikiwamo kuwekewa bunduki kwenye shamba lake kwa lengo la kumchafua.
Vilevile, amesema mbunge huyo ameundiwa kundi la watu ambao wanalipwa pesa na watu wenye nia ovu dhidi yake.
Rais Magufuli alifichua njama hizo jana katika mkutano wa hadhara alioufanya katika Viwanja vya Rujewa wilayani Mbarali ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Mbeya.
“Changamoto nyingine iliyopo Mbarali ni majungu, mtaichelewesha kwenda mbele, ninajua wapo watu ambao wamelipwa hela, wamepangwa kuja kumzomea mbunge, haya hayatawasaidia, ukiwa unataka ubunge, usububiri wakati, subiri uje umshinde kwenye kula, lakini haya majungu yanawachelewesha," alisema.
Rais Magufuli aliongeza: "Majungu hayajengi, ninawaambia ndugu zangu kwa dhati kabisa, mnapochagua watu hamchagui malaika, huyu ni mbunge wa kuwatumikia watu, mmepanga kumchafua, hatachafuka.
"Mmefanya mengi ya ajabu, mkaenda kwenye shamba lake mkaenda kufukia silaha ambazo wala siyo zake kwa umiliki, msifikiri hatujui, acheni mambo ya namna hiyo na bahati nzuri wanaofanya hayo wanajulikana, kama hizo ndizo mbinu za kupata ubunge hupati, mimi ndiyo mwenyekiti."
Rais Magufuli pia aliaziga apewe majina ya watu waliopewa hekta 5,900 ambazo serikali iliagiza zirudishwe kwa wananchi kutoka kwa wawekezaji.
"Ninachotaka hizo hekta nipate orodha ya watu waliopewa, mnipangie orodha, kwamba huyu ni fulani amepewa hekta kadhaa, ili hekta hizi 5,900 zijulikane wamepewa kina nani, inawezekana zikawa hewa.
"Haiwezekani wananchi wote wa Mbarali mimi nimetoa ardhi halafu wao walalamike kwamba hawajapata ardhi wakati mimi nimetoa, isije ikawa zimerudi tena kwa wawekezaji au wamekuja wengine wapya kisirisiri.
"Lengo la yale mashamba yalikuwa si kupewa wawekezaji tena, lengo lilikuwa ni kupewa wananchi kwa ajili ya kulima," Rais Mgufuli alisema.
Kiongozi huyo wa nchi pia aliagiza kutafutwa madalali ambao wamekuwa wakiwawakodishia wananachi mashamba kwa kiwango kikubwa cha fedha ili kulima.
“Mwekezaji wa shamba namba 70 na 78 alipewa kihalali kwa mujibu wa sheria, na alipokuwa na shamba lake amekuwa akilima lakini katika maeneo mengine amekuwa akiwapa watu kwa kuwakodisha, lakini kwa bahati mbaya kuna madalali hapa katikati wamekuwa wakiuza kwa kukodisha kwa Sh. 600,000 mpaka Sh. 700,000, ninaomba watafutwe," aliagiza.
Kabla ya kuhutubia katika viwanja vya Rujewa, Rais Magufuli alisimama mara kwa mara njiani kwa ajili ya kusikiliza kero na kuzungumza na wananchi, akitoa onyo kwa watumishi wasio waamifu ambao wamekuwa wakipewa kusimamia miradi ya serikali na kuiba pesa za serikali.
Rais Magufuli pia alitoa wito kwa watendaji wa serikali kuhaki
0 comments:
Post a Comment