Mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange, amehukumiwa hapo jana kwenda jela kwa wiki 50, kwa hatia ya kukiuka amri ya korti ya Uingereza miaka saba iliyopita.
Assange aliomba hifadhi katika ubalozi wa Equador mjini London, kuepuka kusafirishwa hadi Sweden alikokuwa akikabiliwa na tuhuma za ubakaji, ambayo anayakanusha.
Mfichuzi huyo wa nyaraka za siri ambaye alikamatwa Aprili mwaka huu baada ya kufukuzwa ubalozini alikokuwa akijificha, anakabiliwa pia na kitisho cha kupelekwa Marekani.
Nchi ya Marekani inamtafuta kwa kuvujisha mamilioni ya nyaraka zake za siri. Kesi yake ya kwanza kuhusiana na ombi la Marekani, litasikilizwa leo Alhamis.
0 comments:
Post a Comment