Mfalme anaonekana akimwaga maji ya baraka kwenye kichwa cha Malkia Suthida.
Mfalme wa Thailand amemuoa Naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wake , na kumpa cheo cha malkia, imesema taarifa ya ufalme huo.
Tangazo hilo la kushitukiza limetolewa huku sherehe za kutawazwa kwake zikitarajiwa kuanza Jumamosi, wakati atakapochukua wadhfa wake.
Mfalme Maha Vajiralongkorn, mwenye umri wa miaka 66, alikuwa mfalme kikatiba baada ya kifo cha baba yake aliyependwa sana kilichotokea mwaka 2016.
Amekwisha wataliki wanawake mara tatu na ana watoto saba.
Ufalme ulisema kuwa: Mfalme Vajiralongkorn "ameamua kumpandisha cheo Generali Suthida Vajiralongkorn Na Ayudhya, na kuwa Malkia Suthida na atakuwa na cheo cha kifalme na hadhi kama sehemu ya familia ya kifalme".
Malkia Suthida ni mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn na amekuwa akionekana hadharani pamoja nae kw amiaka mingi, ingawa mahusiano yao haukuwahi kukubalika rasmi.Malkia Suthida alipewa cheo cha Generali mwaka 2016
Picha kutoka kutoka katika sherehe za harusi zilionyeshwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni vya Thailand Jumatano, ambapo watu wa wengine wa familia ya ufalme na washauri wa ufalme walihudhuria.
Mfalme alionekana akimwagia maji ya baraka Malkia Queen Suthida kichwani. Baadae wawiloi hao walisaini cheti cha ndoa.
Mnamo mwaka 2014 Vajiralongkorn alimteua Suthida Tidjai, ambaye ni mhudumu wa zamani wa Thai Airways,kama naibu kamanda wa kikosi cha walinzi wake. Alimpandisha cheo na kuwa Generali kamili jeshini Disemba 2016.
Mfalme aliyetangulia Bhumibol Adulyadej, alitawala kwa miaka 70 na kuwa ndiye mfalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani na alifariki dunia mwaka 2016.
Chanzo - BBC
0 comments:
Post a Comment