Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu (CCM) ametishia kufanya fujo jimboni kwake kama Serikali haitawaondolea kero ya maji.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji jana bungeni jijini Dodoma, Kadutu amesema jimbo lake kwa muda mrefu limetengwa na halipewi kipaumbele huku wananchi wake wakitaabika kwa ukosefu wa maji.
Kadutu ambaye amezungumza kwa hisia, amesema yeye na wananchi wanakwenda kuziba Mto Malagalasi kwa sababu mradi wa Mto huo badala ya kuhudumia pia wananchi wa Ulyankulu, umeelekezwa Kaliua na Urambo mkoani Tabora.
“Mheshimiwa Waziri na wataalam mlioko hapa nyuma yangu hebu fanyeni mnavyoweza, je tutatengwa hadi lini?, sisi sio wakimbizi kama hamtaki kutupa tawala za mikoa tupeni maji, wataalam msikie tutaleta vagi hata wao hawatakanyaga huko,” amesema.
0 comments:
Post a Comment