Watanzania wametakiwa kudumisha amani na upendo uliopo nchini kwani ndiyo zawadi pekee waliyoachiwa na mwenyezi Mungu.
Rai hiyo imetolewa na Nabii Mkuu Wa kanisa la Ngurumo ya Upako Dr. Geordave Kisambale jijini Arusha wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo katika ibada ya Chuo cha unabii iliyofanyika Kosongo jijini humo.
Alisema ni wajibu wa kila Mtanzania kuienzi ,kuidumisha na kuilinda amani iliyopo.
"Unajua Mungu anatupendelea sana Watanzania ametupa amani ya nchi yetu ,ametufanya tunaishi kwa upendo angalieni nchi zingine wanapigana kila siku,kuna vita ndugu kwa ndugu hawapendani lakini sisi watanzania tunaishi kwa amani hivyo ni vyema amani hii tuliyopewa tuilinde kama vile mboni ya jicho letu", alisema Geodave.
Aidha aliwataka watanzania kutoruhusu mtu yeyote yule kuingilia na kuivuruga amani hiyo.
Pia alimtaka kila Mwananchi kupitia imani yake kuendelea kuombea nchi ya Tanzania iendelee kuwa na amani huku akiwa akiwakumbusha kuwaweka katika maombi kila siku viongozi wa kitaifa akiwemo Rais John Pombe Magufuli ili mungu aendelee kuwaongoza na kuwapigania.
Aidha aliwataka Watanzania kutii sheria za nchi bila vurugu, huku akisisitiza wanasiasa kutopandikiza chuki miongoni mwa wananchi badala yake wawaunganishe na kuwafanya kitu kimoja.
Na Woinde Shizza , Arusha
0 comments:
Post a Comment