Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi Nchini limeahidi kushughulika na vitendo vya mauaji vinavyoendelea kutokea mkoani Njombe kwa njia yoyote.
Kamanda wa polisi Nchini IGP Simon Siro akiwa mkoani Njombe kwa ukaguzi wa kawaida, amesema kuwa amezielekeza timu za upelelezi kuhakikisha yeyote atakayehusika na mauaji anapatikana na kushughulikiwa.
“Hali ya uhalifu ipo chini lakini tunashida bado ya mauaji na nimetoa maelekezo kwamba lazima haya tuyamalize mkoa wa Njombe,wale wanaofanya kwa ulevi,kwa ugomvi na kwa ushirikina waache kwasababu wataishia magerezani
"Nimeelekeza timu zetu maalumu za upelelezi kuhakikisha kuwa yule anayefanya mauaji anapatikana, kuna tukio hapa juzi kwasababu ya ushirikina mzee amekamatwa amepasuliwa pasuliwa ni mambo ya kishamba, haiwezekani mkoa mmoja kila siku Njombe mauaji watu hawataki kuacha ”alisema Siro
Katika hatua nyingine kamanda Siro ameliagiza jeshi la polisi mkoa wa Njombe kutoa elimu kuanzia mashuleni mpaka vyuoni juu ya madhara ya ubakaji kutokana na changamoto hiyo kuonekana kuwa kubwa mkoani Njombe.
“Lakini pia nimeona tunashida ya kubaka na makosa haya ya kubaka ni mengi nimeelekeza waende kutoa elimu kuanzia mashuleni kueleza madhara ya kubaka,lakini mbaya zaidi imeonekana kesi ikienda mahakamani makosa mengi ya kubaka yanashirikisha ndugu ,nimesema biashara ya ndugu haipo ukifanya kosa la jinai
"Kwa hiyo unapobaka ujue inakushtaki jamhuri haya mambo ya kizamani tuyaache wanawake mbona ni wengi sana swala kufuata tu sheria”alisema kamanda
Hata hivyo kamanda Siro amesema ili kuimarisha utendaji kazi wa jeshi hilo serikali imetoa fedha takribani bilioni 900 ambazo zimeanza kutumika katika ujenzi wa makazi ya askari hivyo ujenzi unaendelea kwa awamu ili kukamilisha maeneo yote nchini.
0 comments:
Post a Comment