Monday, 29 April 2019

Iran: Marekani lazima iombe idhini kwa jeshi la Iran la SEPAH kuweza kupita Hormuz

...
Mkuu wa Majeshi ya Iran amesema kuwa meli za Marekani haziwezi kupita katika Lango Bahari la Hormuz bila ya kuomba idhini kwanza kutoka kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Meja Jenerali Mohammad Baqeri amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea hadi hivi sasa kuhusu meli za kivita, za kibiashara na za mafuta na vyombo vyote vya majini vya Marekani vinavyopita kwenye Lango Bahari la Hormuz. 

Wakati wowote vinapoamua kufanya hivyo lazima viombe idhini kwanza kutoka kwa jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ndipo vinaweza kupita baada ya kuruhusiwa na jeshi hilo.
 
Amesema Iran inataka lango hilo libakie wazi na salama na kuonya kuwa Tehran haitoruhusu mtu yeyote kuhatarisha usalama wa eneo hilo. 

Itakumbukuwa kuwa karibu thuluthi nzima ya mafuta yanayotumika maeneo mbalimbali duniani yanapitia katika Lango Bahari la Hormuz la nchini Iran. 

Jukumu la kulinda usalama wa eneo hilo muhimu mno kiistratijia ni la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ambalo hivi karibuni rais wa Marekani Donald Trump alidai kuwa  jeshi hilo ni taasisi ya kigaidi.

Mkuu huyo wa vikosi vya ulinzi vya Iran ameongeza kuwa, madhali meli za nchi nyingine zinatumia lango hilo kusafirisha mafuta, Iran nayo ni haki yake kabisa kutumia eneo lake hilo kusafirishia mafuta. 

Hata hivyo amesema hii haina maana kwamba Iran inakusudia kulifunga lango hilo. 

Amesema: "Hatuna nia ya kulifunga Lango Bahari la Horumuz isipokuwa kama adui atatulazimisha kufanya hivyo. Na tukiamua kulifunga, basi tunao uwezo wa kufanya hivyo muda wowote ule."

Credit: Parstoday


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger