Taarifa kutoka mkoani Mara zinasema kwamba Kijana Frank Elias (22) mkazi wa Kakonko mkoani Kigoma, amelazwa hospitali akiwa na hali mbaya baada ya kuchomwa moto na mchungaji wake.
Tukio hilo limetokea Aprili 28 katika kanisa la Cag Calvari katika kijji cha Musati limethibitishwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Jma Ndaki, na kusema kwamba tayari Polisi wameshamkamata mchungaji huyo aliyejulakana kwa jia la Anna Butoke.
Asimulia alivyochomwa moto
Akisimulia tukio hilo jinsi lilivyokuwa, Frank amesema kwamba alienda kanisani hapo kuombewa kwa kuwa anasumbuliwa na kichwa, akaambiwa apige magoti na afumbe macho na kutii, ndipo akamwagiwa mafuta ya taa, alipowashiwa moto, akaanza kuungua huku akiombewa na kuambiwa kuwa mizimu yote itakwisha na atapona.
"Nilianza kuungua huku wao wakizidi kuomba, hali ikawa ngumu nikapiga kelele ndipo wakaanza kuuzima moto huku wakisema hiyo ni nguvu ya Mungu, watu wakaanza kujitokeza nikapelekwa Kituo cha Polisi Kenyana na kukimbizwa hospitali kwa matibabu”, amesema Frank
Naye Mchungaji Anna Butoke amekiri kuwa wao walikuwa wanachoma mikoba ya kijana huyo ajabu akawa anaungua yeye.
"Alifika kujaribu kutaka kuteketeza mchungaji na viongozi wengine lakini akazidiwa nguvu, tukamwambia alete vifaa vyake vya uchawi, tukavimwagia mafuta ya taa na kuwasha moto akiwa amevishika badala ya kuungua vifaa hivyo akawa anaungua yeye nasi tulishangaa”, amesema Mchungaji Anna.
Kamanda Ndani amesema kwamba jeshi la polisi linamshikilia Mchungaji huyo huku wakiendelea na uchunguzi kujua iwapo alishawahi kufanya matukio kama hayo siku za nyuma, na kuwataka wananchi kuwa makini na masuala ya imani kwani mengine yanaweza yakagharimu uhai wao.
0 comments:
Post a Comment