Tuesday 30 April 2019

Rais Magufuli Akataa Ombi la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kuhusu Vyama vya Upinzani

...
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Albert Chalamila amesema,haoni sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi nchini badala yake kuwe na chama kimoja tu kitakachoitwa 'Magufuli Ruling Party'. 

Chalamila ameyasema hayo leo Jumanne, Aprili 30, 2019, wakati akitoa salamu za mkoa wake kwa Rais Magufuli kwenye mkutano wake na wananchi wa Wilaya ya Kyela.

“Mheshimiwa Rais umefanya mengi sana mema kwa nchi yetu, umetoa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo, hapa Kyela umetupatia vitambulisho 10,000, wananchi 8,850 wameshagawiwa vitambulisho hivyo kwa gharama ya shilingi 20,000 kwa kila kitambulisho.

“Katika suala la elimu bure, katika mkoa wa Mbeya unawalipia wanafunzi wa shule za msingi zaidi ya 400,000 na wa sekondari zaidi ya 86,000.  


"Tunakushukuru sana mheshimiwa Rais. Katika mazuri haya unayoyafanya, sioni kama kuna haja ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa, badala yake kuwe na chama kimoja tu kinachoitwa ‘Magufuli Ruling Party’, amesema Chalamila.

Hata hivyo Rais Magufuli ameyakataa maoni hayo na kusema anatamani kuwe na vyama vingi, lakini CCM ishinde wakati wote.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger