Tuesday, 30 April 2019

Rais Magufuli Aelezea masikitiko yake kufuatia timu za soka za taifa Kufungwa na Mataifa Mengine

...
Rais   Magufuli ameeleza masikitiko yake kufuatia timu za soka za taifa ambazo ni timu ya wakubwa (Taifa Stars) na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys,  kufungwa na timu za mataifa mengine katika michuano mbalimbali ambayo imechezwa hivi karibuni.

Magufuli amesema hayo leo Aprili 30, 2019 wakati wakiwahutubia wananchi wa Kyela mkoani Mbeya ikiwa ni siku chache baada ya Serengeti Boys kuondolewa kwenye michuano ya Afcon U17, iliyokuwa ikichezwa hapa nchini na kusema  kitendo cha kufungwa kwa timu hizo kimekuwa kikimnyima raha huku akimtaka waziri wa micghezo, Dkt Harrison Mwakyembe kubeba aibu hiyo ya kufungwa kila mara.

“Kukatika kwa umeme kunaumiza sana, unakuta unaangalia mpira umeme unakatika halafu goli linaingia, na Waziri wa Michezo anatoka huku Mbeya, ingawaje kwenye timu ya vijana ameniangusha sana. Katika vitu ambavyo huwa vinaniudhi ni kufungwa timu zangu, huwa inaniuma mno, yani watu milioni 55, mnafungwa na timu ya nchi yenye watu milioni 33, hii ni aibu kubwa mno.

“Natamani siku moja niwe waziri wa michezo halafu niwaonyeshe mimi ni nani, kwanza kikosi nitakipanga mimi mwenyewe halafu tuone kama tutafungwafungwa tena, timu ya wakubwa nayo hivi karibuni itaanza mashindano, sijui nayo mechi ya kwanza tu itafungwa! Labda kufungwa nao ndiyo mchezo mzuri,” amesema Magufuli.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger