Monday 29 April 2019

Serikali Kuendelea Kulinda Uhuru wa Kuabudu

...
Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa Katiba huku akiwapongeza Watanzania namna wanavyotumia uhuru huo bila kuuvunja.

Pia ameahidi kuwa Serikali itandelea kushirikiana na dini pamoja na madhehebu yote kwa sababu ni taasisi nyeti na muhimu katika jamii kwa sababu zinasaidia kuwafanya wananchi kuwa raia wema.

Ameyasema hayo  jana Aprili 28, 2019 katika misa ya kumsimika Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa kanisa katoliki Jimbo Kuu la Mbeya iliyofanyika katika viwanja vya Sokoine na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Alisema amefurahi kuona katika misa ya kumsimika askofu Nyaisonga kuhudhuriwa na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali huku akiamini pia wahudhuriaji ni kutoka sehemu tofauti.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger