Friday, 5 April 2019

Askari polisi ajiua kwa risasi kisa kukosa mtoto kwa miaka mitano

...
Askari  Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Gideoni Kijelengwa (30), amedaiwa kujiua kwa kujipiga risasi kichwani na kufariki dunia papo hapo kwa madai ya kuishi ndani ya ndoa miaka mitano bila kupata mtoto.

Tukio hilo limetokea jana saa 1:30 asubuhi wakati askari huyo akiwa lindo kwenye benki ya Access Wilaya ya Kahama na kabla ya kujiua alimtumia ujumbe mfupi mkewe kuwa amechoka kuishi, kutokana na kutopata mtoto ndani ya ndoa yao na kuamua kujipiga risasi na kusababisha kifo chake papo hapo.

Akitoa taarifa kwa vyombo habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Richard Abwao, alisema askari huyo alikuwa ameoa mwalimu na baada ya kuona hawaja jaliwa kupata mtoto ndani ya ndoa yao kwa muda wa miaka mitano, ndipo alipoamua kujipiga risasi shingoni ambayo ilisambaratisha kichwa chake.

"Kabla ya kujiua askari huyo alimtumia ujumbe mke wake kuwa amechoka kuishi kutokana na kukaa ndani ya ndoa bila ya kupata mtoto ndani ya miaka mitano, na kwenye ujumbe huo pia alimwonyesha mali za viwanja vilipo na kisha akajipiga risasi na kufariki hapo hapo," alisema Abwao.

Alisema askari huyo ni mkazi wa Muleba mkoani Kagera, na Jeshi la Polisi limeshaanza taratibu za kuusafirisha mwili huo kwenda kwao kwa ajili ya maziko.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger