Na Dinna Maningo,Tarime. Wafanyabiashara katika soko kuu mjini Tarime wamepokea mradi wa ujenzi wa soko kuu jipya utakaogharimu zaidi ya Bilioni 8 fedha zilizotolewa na Serikali kuu huku wakiipongeza Serikali kuwezesha fedha ambazo zitafanikisha kujenga soko la kisasa tofauti na lililopo ambalo limepitwa na wakati. Akizungumza na Wafanyabiashara wa soko kuu viwanja vya shule ya msingi Nyamisangura,Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Tarime,Elias Ntiruhungwa alisema kuwa baada ya kupokea fedha hizo tayali halmashauri imetangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi wa soko ambalo ni jengo la ghorofa litakalokuwa na maduka 419,vizimba…
0 comments:
Post a Comment