Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani, hususan wanaopitiwa na Mradi wa Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuchangamkia fursa hiyo kutokana na unafuu wa gharama zake. Alitoa rai hiyo jana, Februari 15, 2019 kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, kuwasha umeme na kuzungumza na wananchi katika wilaya za Rufiji na Kibiti. Alisema, gharama za uunganishaji umeme wa REA kwa kila mwananchi ni shilingi 27,000 tu lakini pindi mradi huo utakapoisha muda…
0 comments:
Post a Comment