Thursday, 21 February 2019

MBUNGE SUGU BADO AENDELEA KUNG'ANG'ANIWA POLISI

...

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ bado amenga’ang’aniwa na polisi tangu alipokwenda akiitikia wito wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei kwa ajili kuhojiwa.

Sugu amefika ofisi kwa Kamanda Matei saa mbili asubuhi leo Februari 21, 2019 kama alivyotakiwa na baadaye kuhojiwa kuhusu kauli zinazodaiwa kuwa za kichochezi, matusi na dharau kwa mamlaka za Serikali kuhusiana na mchakato wa utoaji wa vitambulisho vilivyotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya wajasiriamali.

Hadi muda huu, Sugu bado yupo mikononi mwa polisi, Makao Makuu ya Polisi Mbeya huku hatima ya kuachiwa ama kutoachiwa ikiwa bado kujulikana.

Kamanda Matei amesema wamemuita Sugu kutokana na mkanda wa video uliosambaa mitandaoni ukimuonyesha akizungumza na wananchi huku akitoa maneno ya uchochezi, kukashifu viongozi wa Serikali na yanayoweza kuhatarisha usalama na ulinzi wa mkoa wa Mbeya.

“Kuna ‘Clip’ inazunguka (mitandaoni) inamuonyesha mheshimiwa Mbunge (Sugu) akiwa kwenye madarasa ya shule au sokoni sijui, lakini akiwa anafuatilia suala zima la vitambulisho vya wajasiriamali.

Na Kahango, Mwananchi
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger