Jamaa mmoja mjini Naivasha nchini Kenya amejitoa uhai baada ya kugundua kuwa mpenzi wake alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki yake wa karibu.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Samuel Kimani, jamaa huyo aliruka mbele ya lori lililokuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi katika barabara kuu ya Nakuru kuelekea Nairobi siku ya Ijumaa.
Taarifa za The Standard Ijumaa Februari 22,2019 zinaeleza kuwa jamaa huyo aliacha kijikaratasi kwenye mfuko wake ambapo alikuwa ameelezea sababu yake kujitoa uhai ambapo alimlaumu mpenzi wake kwa kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao wa kimapenzi.
Alidai kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya mpenzi wake waliopanga kufunga ndoa kwa pamoja kumsaliti kwa kushiriki mapenzi na rafiki wake wa karibu.
"Alielezea kwenye kijikaratasi hicho jinsi alivyokutana na mpenzi wake na wawili hao walikuwa wanapanga kufunga pingu za maisha hivi karibu ila alimpata mpenziwe akishiriki mapenzi na rafiki wake wa karibu," Kimani alisema.
" Marehemu aliwaonya wawili hao dhidi ya kuhudhuria mazishi yake kwani ni wao walimpelekea yeye kujitoa uhai," Kimani aliongezea.
Afisa mkuu wa Naivasha Samuel Waweru alithibitisha kisa hicho na kusema mwili wa mwendazake ulipelekwa katika chumba cha kihifadhi wafu cha hospitali ya kata ndogo ya Naivasha.
0 comments:
Post a Comment