Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ametoa onyo kali kwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Bw. Issai Mbilu ambaye ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara wa Halmashauri hiyo kwa kutotekeleza majukumu yake ipasavyo na kumtaka kuacha kiburi na kujirekebisha mara moja ili atekeleze majukumu yake kwa kutenda haki. Onyo hilo amelitoa wilayani Korogwe wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Dkt.Mwanjelwa amemtaka…
0 comments:
Post a Comment