Watu 19 wameripotiwa kupoteza maisha katika ajali ya lori lililokuwa na mzigo, lenye namba T 388 CAA baada ya gari hilo kufeli breki na kugonga magari mawili likiwemo la abiria katika mteremko wa Senjele Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.
Inadaiwa kuwa lori hilo lilikuwa likitoka Tunduma kuelekea Mbeya na baada ya kufeli breki, lilianguka na kulilalia gari aina ya Coaster lenye abiria lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tunduma katika mteremko huo ambao upo katika eneo la Nanyala mpakani mwa mikoa ya Songwe na Mbeya.
Taarifa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe imesema wamepokea miili 17 ya marehemu wa ajali hiyo ambayo wameihifadhi, na miili mingine miwili (ya waliokuwa majeruhi na baadaye wakafariki dunia) imehifadhiwa katika Hospitali ya Misisi iliyopo Mbeya Vijijini.
0 comments:
Post a Comment