1. Kutumia gari
Hapa jamaa wanakuja na roli kubwa au dogo kisha wanapakia kama yao kisha kutokomea wanakojua wao. Hii haijarishi ka umeiloki ilimradi tu imepaki ambapo huioni.

2. Mtu wa karibu
Aweza kuwa mke, mme,rafiki, jirani au mgeni, anakusoma unalala saa ngapi then wanakuja usiku kitu kinaibiwa.

3. Wizi magetini
Hapa jamaa wanawasoma wale wanaolaza pikipiki getini. Wanaruka ukuta na waya au kamba za manira the wa ndani wanainyanyua then wa nje wanaivuta.



4. Kutumia funguo za kubahatisha
Hapa hutumia trial and errors keys. Funguo inajaribishwa na ikikubari jamaa wanaendesha ka yao.

5. Sabuni
Jamaa wanatembea na sabuni, ukiacha funguo wazi mf mezani bar, dukani, mikutanon n.k wezi wanaichukua na kuikandamiza ktk sabun then wanairudisha. Baada ya hapo wanaipeleka kwa fundi funguo na anaichonga. Wanakulia timing then pikipiki inawekwa ufunguo bandia na inaibiwa (si lazima siku hiyo hiyo)

6. Njia ya abiria
Hapa abiria anajifanya kukodi boda, anakupitisha chocho na anakutishia kisu, bastora au unamwagiwa maji yanayowasha then unaachia pikipiki halafu anaondoka nayo. Wengine huamua kuua kabisa.

7. Utekaji
Hii ni common, wezi wanavizia vichochoroni na kukuteka. Waweza kuuawa au kujeruhiwa na watekaji.

8. Polisi
Waweza kuuza pikipiki zilizokamatwa.

9 Kukokota
Hapa pikipiki ambayo haijafungwa hukokotwa na wezi ka vile ni yao! Hii inazihusu pikipiki zisizolokiwa!

Waweza kuongeza njia nyingine ili tujiepushe na wizi huu unaokua kila uchwao!