HABARI WANAFUNZI 28,037 KUKOSA MIKOPO.
Wanafunzi 28,037 watakosa mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya hivyo watalazimika kusaka njia mbadala kama wanataka kuendelea na masomo hayo. Hadi kufikia julai 31 wanafunzi 58,037 walikuwa wametuma maombi ya mkopo na bodi hiyo imesema ina uwezo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi 30,000 tu. Pia kuhusu madai ya wanafunzi wa vyuo vitano kutaka wapewe bilioni 6.6 kwaajili ya mafunzo ya vitendo, bodi ya mikopo imesema malipo hayo yaandaliwa na kwamba hundi za malipo  hayo zinatarajiwa kupelekwa katika vyuo wiki ijayo. Vyuo hivyo ambavyo havijapata fedha ni SAUT, IFM, Teofilo Kisanji- Mbeya, Tumaini, SMUCCO na Jordan cha Morogoro.