Fid Q akiwa katika pozi
la picha na tabasamu la ukweli baada ya mwana Hip hop bora Tanzania.
Diamond akitoa machache
baada ya kupata Tuzo
Kikundi cha Weusi
wanaotamba na wimbo wa Gere nao hawakuziachia tuzo hivi hivi.
Background
Kilimanjaro Music Awards ni tuzo zinazotolewa kila mwaka kwa wasanii wote nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Hujulikana kama “Kili Music Awards” kutokana na mdhmini wake mkuu ambaye ni Kilimanjaro Premium Lager.
Tuzo huwa zinatolewa kila mwaka kwa dhumuni la kuwapa uwamko wasanii wa Afrika Mashariki, kundeleza vipaji na usia kwa jamii ya kiafrika kwa ujumla, hivyo hupewa kama pongezi kwa kazi walioifanya kwa uelimisha jamii katika kipindi cha mwaka mzima.
Hizi ni tuzo pekee zinazowaenzi wasanii wa aina zote za muziki, zilianzishwa toka mwaka 1999 na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA). Toka wakati huo, tuzo hizi zimekua maradufu na zimedhaminiwa kwa ushirikiano na bia ya Kilimanjaro Premium Lager toka 2003.
Washindi hawapati kutambulika na nafasi ya kuonekana katika vyombo vya habari tu, bali hushinda zawadi za fedha taslimu zinazowasaidia kuendeleza muziki wao. Lengo la Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni kuwahamasisha wasanii kutoka sehemu mbalimbali nchini kufikia kilele cha mafanikio ya kimuziki, kwa kutambua kwamba ndoto zao hazishii ngazi ya kitaifa, bali kimataifa pia.
WASHINDI WA KILLI MUSIC AWARDS 2014
1. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA TANZANIA - Bora Mchawi, Dar Bongo Massive
2. MSANII BORA CHIPUKIZI ANAYEIBUKA - Young Killer
3. WIMBO BORA WA ZOUK - Yahaya, Lady Jaydee
4. WIMBO BORA WA AFRO POP - Number One, Diamond Platnumz
5. WIMBO BORA WA RAGGA / DANCEHALL - Nishai Chibwa Ft Juru
6. WIMBO BORA WA RAGGAE - Niwe na wewe, Dabo
7. WIMBO BORA WA TAARAB - Wasiwasi wako, Mzee Yusuf
8. KIKUNDI CHA MWAKA CHA TAARAB - Jahazi Modern Taarab
9. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB - Isha Ramadhani
10. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB - Mzee Yusuf
11. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI - Ushamba mzigo, Mashujaa Band
12. MWIMBAJI BORA WA KIKE BENDI - Luiza Mbutu
13. MWIMBAJI BORA WA KIUME BENDI - Jose Mara
14. RAPA BORA WA MWAKA BENDI – Furguson
15. BENDI YA MWAKA - Mashujaa Band
16. MWIMBAJI BORA WA KIKE, KIZAZI KIPYA - Lady Jaydee
17. MWIMBAJI BORA WA KIUME, KIZAZI KIPYA – Diamond
18. KIKUNDI CHA MWAKA CHA KIZAZI KIPYA – Weusi
19. WIMBO BORA WA RNB - Closer, Vanessa Mdee
20. WIMBO BORA WA HIP HOP - Nje ya Box, Nick wa Pili Ft Joh Makini & Gnako
21. MSANII BORA WA HIP HOP - Fid Q
22. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHA / KUSHIRIKIANA - Muziki Gani, Nay wa Mitego ft Diamond
23. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI - Tubonge, Jose Chameleone
24. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB - Mzee Yusuf
25. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI - Christian Bella
26. MTUNZI BORA WA MWAKA KIZAZI KIPYA – Diamond
28. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, TAARAB – Enrico
29. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, BENDI – Amoroso
30. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, KIZAZI KIPYA - Man Water, Combination Sound
31. HALL OF FAME, INDIVIDUAL - Hassan BItchuka
32. HALL OF FAME, INSTITUTION - Masoud Masoud
33. VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA - Number One, Diamond
34. WIMBO WA MWAKA - Number One. Diamond
35. MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI - Isha Ramadhani
36. MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME WA MUZIKI - Diamond
CHANZO: www.bongosound.com
0 comments:
Post a Comment