Afrika kama tunavyoifahamu, ilikuwa ni
sehemu ya Mila na Tamaduni bora kabisa, sehemu ambayo heshima adabu
vilikuwa ni msingi wa jamii yake, hasa kwenye jamii.
Ni sehemu ambayo masikini waliishi kwa
mlo mmoja lakini bado waliheshimiana, kuvumiliana na kupendana. Ni
sehemu ambayo binti angekutwa akifanya mambo ya aibu basi wazazi wake
wangenyooshewa vidole kwa malezi mabaya kwa binti yao. Vivyo hivyo kwa
vijana wa kiume. Mambo haya yalipatikana zaidi kwenye nchi nyingi za
kiafrika na Tanzania ni mojawapo.
Ila kwa sasa, Waafrika wengi, hasa
vijana wamezua mijadala mingi inayotokana na mienendo ya tabia zao
zinazopelekea kuvunjika kwa Mila na Tamaduni bara hili…. Kitu kinachozua
maswali juu ya nani wakulaumiwa kwa kuvunjika na kuharibika kwa Mila na
Tamaduni za Afrika…? Mfano mdogo uko kwenye hiyo picha hapo juu, huyu
binti anafunika nywele kwa imani lakini anafunua matiti. Dini, shule,
wazazi, walezi na walimu wameshindwa kukisaidia hiki kizazi. Ni nani wa
kulaumiwa? Kwangu mimi hiki bado ni kichekesho tu!
0 comments:
Post a Comment