Na John Dotto
Mbunge
wa jimbo la Nzega Mkoani Tabora kupitia CCM, Hamis Kigwangala,
ametanabaisha kuwa anatafakari kama anaweza kugombea Urais kwenye
uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha mapinduzi CCM.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua fununu zilizo enea kwenye
baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiibua mijadala mara kwa
mara inayomshawishi kugombea Urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala amesema
anatafakari jambo hilo zito na kuongeza kuwa muda utakapofika
atayazingatia maoni ya wananchi.
Akizungumzia
maelezo kwamba haoni kama ni hatari kwake kutangazwa mapema kwamba
anataka kuwa kugombea Urais ni kujipunguzia sifa katika chama chake, Dk.
Kigwangala alisema yeye hajatangaza kama anataka Urais na wala
hajamtuma mtu kuanza kumfanyia kampeni, kwani watanzania wanaongozwa na
katiba yenye Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hivyo hayo ni mawazo yao
na wana haki ya kufanya hivyo na yeye binafsi hawezi kuwapinga.
Hivi
karibuni kumeibuka mijadala mizito kwenye mitandao ya kijamii na baadhi
ya wanaharakati kutengeneza vuguvugu la kumshawishi Dk. Kigwangala
kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
ifikapo mwaka 2015.
Mijadala
hiyo mizito imeanzishwa katika mitandao ya Internet na simu za mkononi
walio ipachika jina "Citizens for Kigwangala" ambapo katika mijadala
hiyo wamekuwa wakishawishiana na kumwagia sifa Dk Kigwangala kwamba
ndiye kiongozi pekee anayefaa kuwakilisha chama cha Mapinduzi katika
uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya
vijana wamekuwa wakijadili kuwa Dk Kigwangala ndiye anayeweza kuleta
upinzani wa kweli kwa vyama vya upinzani, wakijenga hoja kuwa amekuwa na
misimamo na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha ndani ya vikao vya bunge.
Dk
Kigwangala ni mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, mwenye taaluma ya
udaktari wa tiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge
ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.
0 comments:
Post a Comment