Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.
Na Kadama Malunde - Midrand Afrika Kusini
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula amesema Bara la Afrika limepiga hatua linafanya vizuri katika kuwapa nafasi wanawake kwenye nafasi za uongozi.
Mhe. Nqakula amesema hayo leo Ijumaa Novemba 4,2022 kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake unaoendelea katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini ukiongozwa na mada ‘Uwezeshaji na ushirikishwaji wa wanawake katika utawala’,
“Tunashukuru Barani tunaendelea kufanya vizuri katika kuwapa nafasi wanawake kwenye nafasi za uongozi. Sisi wanawake tunafanya kazi vizuri, Tumeona katika siasa idadi ya wanawake inaongezeka mfano idadi kubwa ya maspika wa bunge kwenye nchi zetu ni wanawake”,amesema Mhe. Nqakula.
“Wanawake washirikishwe katika masuala ya amani kwani panapotokea vurugu wanaoathirika zaidi ni wanawake, wanaoumia zaidi ni wanawake. Bado wanawake hawajajumuishwa katika masuala ya uchumi.
Usawa wa kijinsia unahitaji utashi wa kisiasa. Ni jukumu la wabunge kuhakikisha wanasimamia masuala ya usawa kijinsia yanapewa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa wanawake hawatengwi hivyo wanawake wawe kwenye tabaka la watu wengi”,amesema.
Hata hivyo amesema hali za maisha za wanawake bado hazijaboreshwa, wanawake wanaajiriwa katika nafasi za chini na hata mishahara wanayolipwa wanawake na wanaume tofauti ni kubwa.
"Tunataka pia kuona idadi ya wanawake inaongezeka katika bodi za Mashirika na Makampuni. Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha kuna usawa wa kijinsia katika kila eneo",amesema Mhe. Nqakula.
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.
Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Lucia Doss Passos akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake
Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Lucia Doss Passos (kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake
0 comments:
Post a Comment