Posta masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania akifungua Kongamano la Biashara mtandao na Anuani za Makazi lilioandaliwa na Shirika hilo na kufanyika Leo Jumamosi oktoba 08 , 2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bi. Teddy Njau akisalimiana na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo wakati wa Kongamano la Biashara Mtandao na Anwani za Makazi kuelekea Siku ya Posta Duniani ambapo kilele chake ni tarehe 9 Oktoba 2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, tarehe 08 Oktoba, 2022.
wizarahmth Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Steven Wangwe akimkabidhi t-shirt Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo yenye ujumbe wa mwezi wa elimu ya usalama mtandao alipotembelea banda la maonesho la Wizara hiyo wakati wa kongamano la Biashara Mtandao na Anwani za Makazi lililofanyika leo Oktoba 8, 2022 jijini Dar es Salaam.
******************************
Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Posta duniani kesho tarehe 09/10/2022 Shirika la Posta nchini Tanzania limefanya Kongamano la biashara mtandao na Anuani za Mkazi lililofanyika leo Jumamosi oktoba 8 katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuhamasisha wananchi kufanya biashara mtandao ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknoloji.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Posta masta Mkuu wa Shirika la Posta Macrice Mbodo amesema kuwa Kongamano la biashara mtandao na anuani za makazi lina umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya Taifa.
"Hauwezi kutaja maendeleo yoyote ya taifa hili bila kujua mahali ambapo wananchi wako wapo na wanakua wapi na shughuli zao zinafanyikia wapi kiusalama, na kwa urahisi wa kuwapa huduma zao" amesema Mbodo
Aidha Mbodo ameeleza kuwa lengo lingine la kongamano hilo ni kueleza Mchango wa Shirika la Posta kwenye kuwaonesha Wananchi biashara ya mtandao ipoje
Kuhusu usalama wa duka la Posta mtandao amesema mfumo huo umetengenezwa kwa kushirikiana na umoja wa Posta duniani ambao ni Wakala wa umoja wa mataifa hivyo amewahakikishia watanzia usalama upo na wasiwe na wasiwasi.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa usalama mtandao kutoka Wizara ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi Steven Wangwe amesema kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira salama ya kufanya biashara mtandaoni kwa kutengeneza sera zinazomhakikishia mtumiaji usalama wa kufanya manunuzi katika mtandao.
0 comments:
Post a Comment