Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Pwani, Mwalimu Douglas Mhini
Katibu wa CWT Wilaya ya Bagamoyo, Mwalimu Shaaban Tessua
NA ELISANTE KINDULU,BAGAMOYO
CHAMA Cha walimu Tanzania (CWT) mkoa Pwani kimeiomba Serikali kuangalia upya hatua iliyoichukua ya kuwa na KIKOKOTOO kipya kwa watumishi wake na badala yake wakirudishe kilichokuwa kikitumika awali.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama Cha walimu mkoa wa Pwani, Mwalimu Douglas Mhini alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT wa wilaya ya Bagamoyo ambao Ni wawakilishi wa chama hicho mahali pa kazi katika mkutano mkuu wa kikatiba wa chama cha walimu uliofanyika katika shule ya Sekondari Bagamoyo.
Mwalimu Mhini amesema kuwa kwa upande wa mkoa wa Pwani wamekusudia kupeleka hoja ya kurejeshewa kikokotoo chao Cha zamani kwenye vikao vya juu vya chama hicho na kuiomba mikoa mingine nchini iunge mkono juhudi hizo.
Kati ya vyama 14 vinavyounda shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania(TUCTA), Mwenyekiti huyo alivitaja vyama vilivyoathirika zaidi ni chama Cha walimu, chama kinachoshulikia wafanyakazi wa Serikali za mitaa na kile Cha watumishi wa Serikali kuu.
Mwenyekiti huyo alisema wao CWT wana mapendekezo mawili aidha kikokotoo Cha awali kirudi au kipya kiendelee lakini huku walimu wakinufaika na posho za kufundishia ,pisho ya nyumba pamoja na posho zingine wanazopata watumishi wengine wa kada za umma.
Awali Katibu wa chama hicho Wilaya ya Bagamoyo Mwalimu Shaaban Tesua aliwashauri walimu kufungua akaunti katika benki ya MCB, kwaajili ya kujiwekea akiba zao pamoja na stahiki mbalimbali za kichama ambazo zitapitia kwenye benki hiyo.
Naye Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Bagamoyo mwalimu Hamisi Kimeza amewataka walimu kujenga mshikamano kwani mshikamano ndio silaha ya kudai haki mahala popote duniani.
0 comments:
Post a Comment