Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Chimbende (34), mkazi wa mtaa wa Majengo Manispaa ya Mtwara Mikindani anadaiwa kuuawa na Himid Mikidadi (23) mkazi wa Kisutu B, baada ya mtuhumiwa kushindwa kulipa pesa ambayo alikula mayai na kushindwa kulipa pesa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo, amesema kwamba tukio hilo limetokea Oktoba 23 mwaka huu na kwamba mauaji hayo yalitokea baada ya marehemu kukataa kulipa pesa ya mayai aliyoyala.
"Kijana huyo alifariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani upande wa kushoto na Himid, baada ya kula mayai yaliyokuwa yanauzwa katika eneo hilo na kukataa kulipa fedha," amesema Kamanda Katembo.
Kaimu Kamanda pia akaeleza tukio la kuuawa kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mohamed Hamis mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Mawindi, Kata ya Mkunwa, ambaye alidaiwa kuuwa na watu wasiofahamika.
Chanzo - EATV
0 comments:
Post a Comment