Wednesday, 26 October 2022

TBS YATEKETEZA BIDHAA ZA JUISI NA MAFUTA YA KUPIKIA HANDENI TANGA

...

**************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kaskazini limekamata na kuteketeza bidhaa za juisi na mafuta ya kupikia zilizokwishwa muda wake wa matumizi ( expired products) zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano za Kitanzania (1.5 milioni).

Bidhaa hizo ambazo hazikuwa salama kwa matumizi zimeteketezwa mapema leo katika dampo la Kwenjugu wilaya ya Handeni mkoani Tanga .

TBS inatoa rai kwa wananchi kuzingatia kusoma taarifa zilizopo katika vifungashio vya bidhaa na kutoa taarifa kupitia namba ya bure 0800110827 pindi wanapopata changamoto yoyote katika bidhaa.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger