Mwanaume wa Iran, Amou Haji.
Mwanaume wa Iran, Amou Haji ambaye anashikilia rekodi ya kuwa ni mtu mchafu zaidi duniani kwa muda wa nusu karne amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, Haji hakuoga kwa takribani miaka 67 na mara kadhaa alishinikizwa kuoga na kupewa maji safi ambapo jaribio hilo lilimhuzunisha sana.
Baada ya majaribio kadhaa kumtaka kufanya hivyo, hatimaye akakubali na baada ya muda mfupi akaugua na kufariki dunia siku ya Jumapili katika kijiji cha Dejgah nchini Iran.
Enzi za uhai wake, Haji alifanya mahojiano na gazeti la Tehran Times mwaka 2014 na kueleza kuwa alikuwa anaishi katika shimo la ardhini na kibanda cha matofali kilichojengwa na wakazi wa kijiji cha Dejgah.
Alipohojiwa kuhusu kuoga, Haji alifuguka kukataa kuoga na kusema kuwa hajatumia maji na sabuni kwa takribani miaka 67, hivyo anahofu huwenda akapata ugonjwa.
Haji alikiambia kituo hicho kwamba uamuzi wake umetokana na vikwazo vya kihisia wakati alipokuwa mtoto mdogo.
Aidha, Haji ameeleza chakula anachokipenda zaidi ni Nungu na nyama iliyooza pamoja na maji machafu huku akibainisha ngozi yake kuzibwa na matope pamoja na usaa.
0 comments:
Post a Comment