Friday, 21 October 2022

NCHI 47 KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA YA UTANASHATI NA UREMBO KWA VIZIWI TANZANIA

...

MATUNDA ya filamu ya The Royal Tour yanaendelea kushamiri baada ya Tanzania kuwa mwenyeji wa shindano la Dunia la utanashati, urembo na mitindo wanaume na wanawake kwa watu wenye changamoto ya usikivu.

Shindano hilo linalotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa ws Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na wanahabari kambini hoteli ya Peackock Mkurugenzi idara ya Maendeleo ya sanaa Dkt.Emmanuel Ishengoma amesema Tanzania kama nchi mwenyeji wa Mashindano makubwa ya utanashati, urembo na mitindo bora ya dunia wamejipanga kwa maandalizi ya awali kuanzia washiriki pamoja kwani maandalizi ya awali yalianza mapema tangu mwezi agosti mwaka huu katika chuo cha sanaa cha Bagamoyo (Tasuba).

Hata hivyo Ishengoma amefafanua kuwa tayari idara ya uhamiaji imeanza kupokea wageni kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kuanza kuwasili kambini kusubiri fainali rasmi ambayo inatarajiwa kufanyika octoba 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.


Aidha amesema washiriki wanaowakilishi nchi ya Tanzania wapo washiriki 6 ambapo walifanya vizuri kwenye ngazi ya Mashindano ya Afrika , wanawake wakiwa 4 na wanaume wawili ambapo Serikali imewapa ushirikiano mkubwa kuanzia gharama zote wawapo kambini hadi kuisha kwa shindano hilo.

Aidha, Shindano hilo limeshirikisha nchi 47 huku Tanzania ikiwa Mwenyeji wa Shindano hilo.

Kwa upande wake Mshiriki wa Shindano hilo ambae pia ni Mshindi wa pili wa ngazi ya Afrika Carolyne Mwakasasa ametoa ushauri kwa vijana ambao wana ulemavu wa kusikia wajitokeze kwa wingi kushiriki mashindano mbalimbali wasione aibu.

"Wajitokeze kushiriki mashindano mbalimbali ili kuweza kuonyesha uwezo wao katika jamii."

Hata hivyo Mwakasasa amesema amejipanga vizuri na anaamini ataipeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika Mashindano hayo ya dunia.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger