Saturday, 15 October 2022

AMFUATA MKEWE KAZINI KISHA KUMUUA KISA HATAKI WARUDIANE

...

 Mwanaume mmoja amemfuata mke wake kazini eneo la Mai Mahiu na kumuua baada ya mwanamke huyo kukataa ombi lake la kurudiana naye.


Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai nchini Kenya (DCI), mshukiwa alimuua Veronicah Wanjiru baada ya kugundua kuwa hakuwa tayari kwa maridhiano.

Ripoti ya DCI inasema kuwa mshukiwa alijaribu kujiangamiza kwa kujidunga lakini hakufanikiwa, kwa sasa akiwa amelazwa hospitalini.

Idara hiyo inasubiri mshukiwa apone kabla ya kumfikisha mahakamani kwa mashtaka ya kumuua mke wake.

Wanjiru alishambuliwa katika eneo la burudani la Club 8 alikofanya kazi ya usafi.

“Wanjiru alikuwa akisafisha eneo hilo, mumewe alipofika na kumwomba kusuluhisha mzozo wao na warudiane lakini akakataa,” taarifa ya DCI inasema.

Baada ya ombi lake la kurudiana kukataliwa, mwanamume huyo alichomoa kisu cha kukata mboga alichokuwa nacho mfukoni.

Alimdungadunga mwendazake mara kadhaa shingoni na kumuua papo hapo.

“Kisha akaamua akaamua kujidunga kwa kisu hicho. Alijidunga kwenye mbavu zake kwa lengo la kujiua. Hata hivyo, hakufanikiwa kujiangamiza,” DCI inasema.

Kwa sasa mshukiwa amelazwa katika hospitali ya Mai Mahiu akiwa katika hali mahututi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger