Mwanafunzi wa darasa la 8 katika Shule ya Msingi ya Nkararo huko Transmara, Kaunti ya Narok, yuko mbioni baada ya kumpiga mwalimu wa zamu kofi alipotaka kuona kazi yake ya ziada.
Inasemekana mwalimu huyo anayefahamika kama Charles Miruka alitokwa na damu na kupoteza miwani yake.
Katibu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu nchini (KNUT) Collins Oyuu alikashifu kisa hicho na kuwataka polisi kumtafuta na kumkamata mwanafunzi huyo.
Mwalimu huyo alikimbizwa hospitalini eneo hilo ambako alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku mwanafunzi huyo akitoroka na bado hajapatikana.
Katibu huyo wa KNUT alitoa wito wa kukamatwa mara moja kwa mshukiwa anayedaiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 18.
"Tunatoa wito kwa polisi kumkamata mara moja mtuhumiwa. Kwa nini mwalimu anapokosewa hakuna anayechukulia suala hilo kwa uzito? Tunaiomba serikali kuwapa ulinzi wa hali ya juu walimu wote nchini" alisema Bw. Korir.
0 comments:
Post a Comment